Majukumu ya Msingi
Majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi yameainishwa katika Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kama ifuatavyo:
(i) Kusimamia na Kuratibu Uandikishaji wa Wapiga Kura katika Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano;
(ii) Kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Uchaguzi wa Rais na Wabunge;
(iii) Kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya Uchaguzi wa Wabunge;
(iv) Kusimamia na kuratibu uandikishaji wa Wapiga Kura na uendeshaji wa Uchaguzi wa Madiwani; na
(v) Kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.
Majukumu mengine ya Tume kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge ni pamoja na yaliyotajwa katika kifungu cha 4C cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, ambayo ni:-
(i) Kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa nchi nzima, kuratibu na kusimamia watu wanaotoa Elimu hiyo; na
(ii) Kuteua na kuwatangaza Wabunge na Madiwani Wanawake wa Viti Maalum.