Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
?Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 67 za wagombea ubunge na udiwani na kuwarejesha wagombea 45 wa ubunge na diwani katika majimbo na kata mbalimbali nchini.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imezitaka asasi za kiraia zilizopata vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura Tanzania Zanzibar, kutumia vibali hivyo kutoa elimu hiyo badala ya kuchanganya elimu ya mpiga kura na kampeni za vyama vya siasa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu ya Mpiga Kura na Asasi za Kiraia Mhe. Balozi Omari Mapuri amesema lengo la kuundwa kwa kamati hiyo ni kuhakiki kuwa elimu ya mpiga kura inayotolewa kwa wapiga kura ni ile iliyokusudiwa na Tume ili iwawezeshe wapiga kura kuwachagua viongozi wakiwa na taarifa sahihi.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepokea rufaa 557 kutoka kwa wagombea ubunge na udiwani Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020 kufuatia kutoridhishwa na uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi katika ngazi ya jimbo na kata.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wasimamizi wa uchaguzi kuwepo kwenye ofisi zao kesho wakati wote wa kupokea fomu za uteuzi kutoka kwa wagombea ubunge na udiwani kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni na iwapo hawatakuwepo ofisini kwa muda huo Tume itachukua hatua kali dhidi yao.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa fomu za uteuzi kwa mgombea wa kiti cha Rais kutoka Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Ofisi za Tume zilizopo Njedengwa jijini Dodoma.