Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka Wasimamizi wa Uchaguzi kuzingatia kanuni,sheria na miongozo ya Uchaguzi wanaposimamia na kutekeleza majukumuya uchaguzi.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo katika Jimbo la Temeke, Mkoani Dar es Salaam na kwenye Kata 46 za Tanzania Bara.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewaonya Wasimamizi wa Uchaguzi ambao ama kwa kujua au kwa makusudi wataharibu au kukiuka taratibu za Uchaguzi kutokana na kutofuata sheria na taratibu za Uchaguzi.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo kwenye majimbo mawili na kata 26 za Tanzania Bara.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewasihi wapiga kura wote wanaoishi kwenye Jimbo la Liwale mkoani Lindi na kata nne za Tanzania Bara, kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Jumamosi Oktoba 13
Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Oktoba 13 mwaka huu katika jimbo la Liwale na kwenye Kata 37 za Tanzania Bara wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni za uchaguzi.