Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 32 zilizopo kwenye Halmashauri 20 za Tanzania Bara, utakaofanyika Juni 15 mwaka 2019.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa madiwani kwenye kata sita (6) zilizopo kwenye halmashauri sita (6) katika mikoa sita (6) ya Tanzania Bara.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia Kuandikisha Wapiga Kura kwa majaribio katika Kata za Kibuta na Kihonda kuanzia Machi 29 hadi Aprili 4 mwaka huu.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesisitiza kuwa itashirikisha wadau wa uchaguzi hususan Vyama vya Siasa katika kila hatua inayopitia kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwaka 2020.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa wito kwa wapiga kura kwenye uchaguzi mdogo wa kata tatu utakaofanyika kesho (Jumamosi: 19.01.2019) kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kuwachagua viongozi wanaowataka wawaongoze kwa kipindi kilichobaki kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi mdogo wa kata mbili utakaofanyika tarehe 19 Januari 2019 sanjari na uchaguzi mdogo wa Jimbo la Temeke na Kata 46 za Tanzania Bara uliotangazwa awali.