Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Ujumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho (IEC Lesotho) umemtembelea Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda shambani kwake Zinje Jijini Dodoma na kujionea shughuli za kilimo na ufugaji zinazofanyika kwenye shamba hilo.
?Ujumbe wa watu wa tatu kutoka Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho (IEF Lesotho) ukuingozwa na Mjumbe wa Tume hiyo,Dkt. Karabo Mokobocho Monlakoana upo nchini kwa ziara ya mafunzo ambapo wametembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaapisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele na Mjumbe wa Tume hiyo Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko baada ya kuwateua kushika nyadhifa hizo tarehe 27 Desemba mwaka 2022.
Mgombea Ubunge Jimbo la Ngorongoro kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bw. Emmanuel Lekishon Shangai ametangazwa mshindi kwa kupata kura 62,017 Kati ya kura halali 62,461 katika Uchaguzi Mdogo wa jimbo hilo uliofanyika tarehe 11 Desemba, 2021.
Taarifa ya Tathmini ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2020
?Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Nagy Kaboyoka, imetembelea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuona Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika eneo la Njedengwa Jijini Dodoma.