Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Maonyesho ya wakulima nanenane kwa Kanda ya Mashariki yanaendelea Katika viwanja vya Nanenane Mjini Morogoro na idadi kubwa ya Wanafunzi wanatembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi kujifunza maswala mbali mbali ya Uchaguzi .
Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa leo, ametembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika maonyesho ya Nanenane mjini Morogoro.
Mtendaji Mkuu Wakala wa Majengo Nchini (TBA) Bwana Elius Mwakalinga ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuendesha Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kwa mafanikio makubwa na kuivusha nchi kwa Salama na Amani.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewataka wanachi kuondokana na mawazo potofu kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi sio huru tu kwakuwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume huwa wanateuliwa na Rais aliyeko madarakani.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Majaliwa Kassim Majaliwa ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuandaa kusimamia na Kuendesha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2015 kwa amani na utulivu.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inashiriki katika maonyesho ya SabaSaba ili kuwapa fursa Wapiga Kura na Wananchi kwa ujumla kupata Elimu ya Mpiga Kura sambamba na kutoa maoni yao yatakayowezesha kuboresha Chaguzi zijazo.