Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
?Wapiga Kura 74,642 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 13 za Tanzania Bara kesho Julai 13,2023.
?Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Makete Bw. William Makufwe amewataka wasimamizi wa vituo vya kupigia kura katika Kata ya Kinyika kuelewa mafunzo na kuyazingatia watakayofundishwa bila ya kukosea ili kuepuka kuvuruga Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika kata hiyo unaofanyika Julai 13, 2023.
Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo tarehe 22 Juni, 2023, wamechangia chupa 14 za damu na kufanya usafi wa mazingira katika kituo cha Afya Makole kilichopo jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma nchini ambayo hufanyika kila mwaka kuanzia tarehe 16-23 juni.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewataka wasimamizi wa uchaguzi wa kata zinazofanya uchaguzi mdogo wa madiwani kuhakikisha wanaongozwa na Katiba, Sheria za Uchaguzi na Maelekezo ya Tume katika kutekeleza majukumu yao ili kusimamia uchaguzi huru, wa haki na unaoaminika.
?Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewataka Masimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata kuvishirikisha vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi katika masuala ya kiuchaguzi ambayo wanastahili kushirikishwa ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika kata 14 za Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 13 Julai mwaka 2023.