Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
?Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imezindua rasmi programu ya utoaji wa Elimu mpiga kura endelevu nchini, kwa kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana ya Songe iliyoko nje kidogo ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeanza kutekeleza programu endelevu za kutoa elimu ya mpiga kura ili kuwaelimisha wananchi waliofikisha umri wa kupiga kura kutekeleza wajibu na haki waliyonayo kikatiba ya kupiga kura katika chaguzi zijazo.
Tanzania imepongezwa kwa kufanikisha kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 kwa amani na Utulivu mkubwa licha ya ushindanimkubwa wa kisiasa uliojitokeza kwenye Uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva leo amemtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai nyumbani kwake Jijini Dar es Salam na kumjulia hali baada ya kurejea kutoka nchini India alikokwenda kwa ajili ya matibabu.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani Kombwey ametembelea banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi lililopo katika viwanja vya J.K. Nyerere mjini Morogoro na kushiriki katika utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura kwa wadau mbalimbali wa Uchaguzi.
Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wameendelea kuelimisha wananchi juu ya maswala ya Uchaguzi kwa kutumia vyombo vya habari vya Mkoani Morogoro sambamba na kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye banda la Tume liloko kwenye viwanja vya Nanenane mjini Morogoro.