Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaapisha Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Mary Longway na Wakili wa kujitegemea Mheshimiwa Asina Omary kuwa Makamishna waTume ya Taifa ya uchaguzi.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo imekabidhi kwa Polisi Daftari la Wapiga Kura lenye majina ya watu wapatao 52,078 ambao walijiandikisha zaidi ya mara mbili katik azoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambalo lilifanyika nchi nzima kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu Oktoba 25, mwaka huu.
Tume ya Taifa ya uchaguzi Makao makuu, hapo kesho inatarajiwa kupokea fomu za uteuzi za vyama 13 kwa ajili ya uteuzi wa nafasi ya kugombea urais kwa ajili ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika hapa nchini mwezi oktoba mwaka huu.
Vyama vya Siasa 21 vinavyotarajiwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani baadaye Mwaka huu vimesaini Maadili ya Uchaguzi yatakayotumika wakati wa kampeni, kupiga Kura na wakati wa kutangaza matokeo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kuahirishwa kwa tarehe ya kuanza kwa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Mikoa ya Dar es salaam na Pwani hadi hapo itakapotangazwa tena.
Citizens have shown a great response on the registration; we did not expect the number of people to be this high. This is the response we expect to meet in other regions,” Pinda said.