Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeahirisha uchaguzi wa kata ya Saranga jijini Dar es Salaam na jimbo la Kwela halmashauri ya Sumbawanga
Tume ya Tiafa ya Uchaguzi imeanzisha kituo cha Mawasiliano “Call Center” ili kuweza kuwasaidia wadau wetu wa Uchaguzi hasa Wapiga kura kuweza kupata Elimu ya Mpiga Kura.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza kuahirisha kampeni za uchaguzi wa Bunge katika jimbo la Handeni Mjini kufuatia kifo cha Mgombea Ubunge Jimbo la Handeni Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ( CCM) Dr. Abdallh O. Kigoda.
Wasimamizi wa Uchguzi nchini wametakiwa kusimamia sheria katika kutekeleza majukumu yao ya kusimamia Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25,2015 mwaka huu
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewataka wanawake nchini kuelimisha Wapiga Kura juu ya masuala muhimu yanayohusu Uchaguzi na kutoegemea Chama chochote cha Siasa.
Mwenyekiti waTume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewataka wagombea na viongozi wa vyama vya siasa kutumia muda mwingi kunadi ilani za vyama vyao na kuwa makini na kauli wanazotoa ili kuepusha kuleta tafsiri tofauti na kile kilichokusudiwa.