Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka Vyama vya Siasa na wagombea watakaoshiriki Uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani visiwani Zanzibar kuzingatia Sheria , Kanuni, Taratibu na Maadili ili Uchaguzi huo uwe huru na wa haki na kuwawezesha wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imepokea ujumbe Taasisi ya Tume za Uchaguzi Duniani (AWEB) uliokuja kujifunza na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya uendeshaji Uchaguzi.
Mkurugenzi wa wa Huduma za Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe amesema kuwa wananchi hawawezi kumwajibisha kwa kumwondoa madarakani Mbunge au Diwani waliyemchangua.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhani amewaasa Watendaji wa Tume kuzingatia maadili katika utendaji pamoja na utekelezaji wa maamuzi yanayofanywa katika vikao mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa Tume.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa Elimu ya mpiga Kura katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Songea mkoani Ruvuma na kueleza umuhimu wa elimu hiyo katika kuwawezesha wananchi na wadau wa uchaguzi kufahamu taratibu na hatua zote za uchaguzi hadi kutangazwa kwa matokeo.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi imesema haitasita kuifutia kibali cha kutoa Elimu ya Mpiga Kura Asasi yoyote itakayotoa maneno ya kuleta uchochezi au kupigia kunadi sera za chama chochote cha siasa kwani kufanya hivyo ni kukiuka matakwa ya Kisheria.