Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekishauri Chama cha ACT – Wazalendo na Vyama vingine vyenye wagombea wa Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Dimani na Udiwani katika Kata Ishirini (20) za Tanzania Bara ,kuwasilisha malalamiko ya ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi kwenye Kamati za Maadili zilizo katika maeneo yao.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wagombea na Vyama vya Siasa vinavyoendelea na kampeni za Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Madiwani kufanya kampeni za kistaarabu zinazozingatia maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2015 na kwamba Chama au mgombea atakayekiuka maadili hayo atachukuliwa hatua.
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI imewataka Wasimamizi wa Uchaguzi, mdogo wa Udiwani katika Kata 20 za Tanzania Bara na Ubunge katika jimbo la Dimani Visiwani Zanzibar kuzingatia Sheria, Kanuni na Maadili ili Uchaguzi huo uwe Huru na wa Haki.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetoa maamuzi ya Rufaa za Mapingamizi mbalimbali yaliyowasilishwa na Wagombea wa Ubunge na Udiwani kutoka katika Vyama mbalimbali vinavyoshiriki uchaguzi mdogo utakaofanyika Januari 22, 2017.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemwapisha Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage kuwa Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) akichukua nafasi ya Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva ambaye amestaafu kwa mujibu wa Sheria.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Jaji Semistocles Kaijage kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) .