Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwepo kwa nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho Mhe. Dr. Elly Marko Macha aliyefariki tarehe 31 Machi 2017.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage amewataka watumishi wa tume hiyo wazingatie maadili na kanuni za utawala bora ili kutekeleza kwa ufanisi jukumu la Tume katika kukuza na kuimarisha demkorasi na utawala bora nchini.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewatahadharisha watu wanaochukua kadi za kupigia kura za wenzao na kuzizuilia au kubaki nazo kuwa ni kinyume cha Sheria.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevihimiza vyama vya siasa kutoa elimu ya mpiga kura kwa wapiga kura na wanachama wao bila ya kuegemea itikadi ya vyama vyao kwani sio wote wanaowaelimisha ni wanachama wao.
Wananchi wa Jimbo la Dimani visiwani Zanzibar leo wamejitokeza kwa wingi katika vituo mbalimbali kupiga kura kumchagua Mbunge atakayewaongoza kwa kipindi cha miaka miaka 4.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji (R) Semistocles Kaijage amesema kila kitu kiko sawa tayari kwa uchaguzi mdogo wa kumpata diwani wa kata ya Ngh’ambi iliyoko katika halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma.