Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (R) Semistocles Kaijage amewataka wasimamizi wa uchaguzi mdogo wa madiwani kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi ili kuepuka kuisababishia serikali hasara.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhan amewaasa wadau wa uchaguzi kuhakikisha kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani utakaofanyika katika Kata 43, Novemba 26 unafanyika kwa amani na utulivu.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani katika kata 43 kuwa utafanyika Novemba 26 mwaka huu.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeendelea na utaratibu wa kutoa elimu ya mpiga kura kila wakati kuhakikisha kuwa Watanzania wanakuwa na uelewa mpana kuhusu masuala ya uchaguzi nahatimaye waweze kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemteua Ndugu Rehema Juma Migilla kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) ,kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Hindu Hamisi Mwenda aliyefariki dunia Septemba 1, 2017.
MKURUGENZI wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhan amevitaka vyombo vya Habari vya Tanzania viige mfano wa wenzao wa Kenya kwa kutumia muda mwingi kutoa Elimu ya Moiga kura.