Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Wapiga kura 216,282 walioandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kupiga kura tarehe 19 Septemba, 2023 kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali na kata sita za Tanzania Bara.
Wagombea 58 kutoka vyama 17 vya siasa vyenye usajili kamili wameteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwania nafasi wazi ya Ubunge kwenye Jimbo la Mbarali lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na kata sita za Tazanzania Bara.
?Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbarali Mkoani Mbeya Bw. Missana Kwangura amefanya uteuzi wa wagombea kutoka vyama 13 vya siasa kuwania kiti cha Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Mbarali unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Septemba mwaka 2023.
Vyama vitano vimechukua fomu za uteuzi kuwania Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Mbarali Mkoa wa Mbeya
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewakumbusha Wasimamzi wa Uchaguzi kutekeleza wajibu wao kwa kuhakikisha kwamba ajira za watendaji wa uchaguzi zinazingatia sifa na uwezo.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Mbarali na Kata 6 za Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 19 Septemba mwaka 2023.