Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 50 za wagombea ubunge na udiwani ambapo kati ya rufaa hizo 4 ni za wagombea ubunge na 46 ni za wagombea udiwani.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 46 za wagombea udiwani waliowasilisha rufaa zao Tume kutoka kata mbalimbali nchini.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 60 kati ya hizo rufaa 2 ni za wagombea ubunge na 58 ni za wagombea udiwani katika kikao chake cha jana tarehe 10 Septemba 2020.
?Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 67 za wagombea ubunge na udiwani na kuwarejesha wagombea 45 wa ubunge na diwani katika majimbo na kata mbalimbali nchini.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imezitaka asasi za kiraia zilizopata vibali vya kutoa elimu ya mpiga kura Tanzania Zanzibar, kutumia vibali hivyo kutoa elimu hiyo badala ya kuchanganya elimu ya mpiga kura na kampeni za vyama vya siasa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu ya Mpiga Kura na Asasi za Kiraia Mhe. Balozi Omari Mapuri amesema lengo la kuundwa kwa kamati hiyo ni kuhakiki kuwa elimu ya mpiga kura inayotolewa kwa wapiga kura ni ile iliyokusudiwa na Tume ili iwawezeshe wapiga kura kuwachagua viongozi wakiwa na taarifa sahihi.