Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Tume ya Taifa ya Uchaguzi
?Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mbarali, Bw. Missana Kwangura amemtangaza Bi. Bahati Ndingo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa kiti cha Ubunge wa Jimbo hilo baada ya kupata kura 44,334 kati ya kura 56,095 halali zilizopigwa kwenye vituo 490 vya kupigia kura.
?Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele leo tarehe 19 Septemba, 2023 ametembelea na kukagua zoezi la kupiga kura kwenye Jimbo la Mbarali lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Wapiga kura 216,282 walioandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kupiga kura tarehe 19 Septemba, 2023 kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali na kata sita za Tanzania Bara.
Wagombea 58 kutoka vyama 17 vya siasa vyenye usajili kamili wameteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwania nafasi wazi ya Ubunge kwenye Jimbo la Mbarali lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na kata sita za Tazanzania Bara.
?Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbarali Mkoani Mbeya Bw. Missana Kwangura amefanya uteuzi wa wagombea kutoka vyama 13 vya siasa kuwania kiti cha Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Mbarali unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Septemba mwaka 2023.
Vyama vitano vimechukua fomu za uteuzi kuwania Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Mbarali Mkoa wa Mbeya