• English
  • |
  • Maswali yaulizwayo Mara kwa Mara   |  
  • Staff Mail

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Uchaguzi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Wajumbe wa Tume
    • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Jinsi NEC Ilivyoanzishwa
  • Uchaguzi
    • Mifumo ya Uchaguzi
    • Mzunguko wa Uchaguzi
    • Uchaguzi Mkuu
    • Uchaguzi Mdogo
    • Matokeo ya Uchaguzi Mkuu
  • Machapisho
    • Sheria za Uchaguzi
    • Ripoti
    • Kanuni za Uchaguzi
    • Maadili ya Uchaguzi
    • Rufaa za Uchaguzi Mdogo 2021
    • Miongozo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020
    • Orodha ya Matokeo ya Rufaa za Ubunge zilizoamuliwa na Tume
    • Wagombea waliopita bila kupingwa
    • Wagombea katika Uchaguzi Mkuu 2020
    • Wabunge na Madiwani Wateule wa Viti Maalum Uchaguzi Mkuu 2020
    • Jarida la Tume kuhusu Uchaguzi Mkuu 2020
    • Mpango Mkakati wa NEC 2021/2022 – 2025/2026
    • Kura ya Maoni
    • Maelekezo
    • Orodha ya Majimbo na Kata
  • Wapiga Kura
    • Elimu ya Mpiga Kura
    • Takwimu za Wapiga Kura
    • Vituo vya Uandikishaji
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • NEC Online TV
    • Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Ratiba ya Kampeni za Wagombea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020
    • Voters Interaction System
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida la Tume la Uchaguzi Mkuu 2020
  • Zabuni/Mnada
    • Zabuni za Ndani
    • Zabuni za Kimataifa
  • Mawasiliano
  • Jarida la Uchaguzi

Wapiga kura 216,282 kupiga kura uchaguzi mdogo wa Mbarali na kata sita

Imewekwa: September 19, 2023

Wapiga kura 216,282 walioandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kupiga kura tarehe 19 Septemba, 2023 kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbarali na kata sita za Tanzania Bara.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele ameyasema hayo Wilayani Mbarali, Mkoani Mbeya leo tarehe 18 Septemba, 2023 wakati akisoma risala kwa ajili ya uchaguzi huo na kuongeza kwamba uchaguzi utahusisha vituo 580 vya kupigia kura.

“Katika uchaguzi huu kuna jumla ya wapiga kura 216,282 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao watashiriki kuchagua viongozi wao. Aidha, uchaguzi huu utahusisha vituo 580 vya kupigia kura vilivyobainishwa,” amesema Jaji Mwambegele.

Kata zenye uchaguzi ni; Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mfaranyaki iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Songea, Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Old Moshi Magharibi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na Mtyangimbole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.

Mwenyekiti wa Tume amevikumbusha vyama vya siasa, wagombea, mawakala wa vyama, wapiga kura na wananchi kwa ujumla kuhakikisha kwamba hawapigi kampeni siku ya kupiga kura kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

“Alama za vyama vya siasa zinazoashiria kampeni kama vile vipeperushi, bendera na mavazi haviruhusiwi kutumika kesho tarehe 19 Septemba, 2023 ambayo ni siku ya uchaguzi,” amesema.

Jaji Mwambegele ameongeza kwamba zoezi la kupiga kura katika maeneo yote ya uchaguzi litafanyika katika vituo vile vile vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Ameongeza kwamba vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa moja kamili (1:00) asubuhi na kufungwa saa kumi kamili (10:00) jioni.

“Iwapo, wakati wa kufunga kituo watakuwepo wapiga kura katika mstari ambao wamefika kabla ya saa kumi kamili (10:00) jioni katika mstari na hawajapiga kura, wataruhusiwa kupiga kura. Mtu yeyote hataruhusiwa kujiunga katika mstari wa wapiga kura baada ya saa kumi kamili (10:00) jioni,” amesema.

Jaji Mwambengele amebainisha kwamba watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale tu ambao wamo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwenye kata husika na wana kadi zao za mpiga kura.

Ameongeza kuwa, hata hivyo, Tume kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 61(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 pamoja na kifungu cha 62(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 imeruhusu wapiga kura ambao wamepoteza kadi zao au kadi kuharibika kutumia vitambulisho mbadala.

“Mojawapo ya kitambulisho mbadala ambacho mpiga kura anaweza kutumia ni Pasi ya Kusafiria, Leseni ya Udereva au Kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),” amesema.

Mwenyeki wa Tume amesisitiza kwamba ili mpiga kura aruhusiwe kutumia kitambulisho mbadala ni sharti awe ameandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na jina lake lipo katika orodha ya wapiga kura katika kituo anachokwenda kupiga kura.

“Katika kituo cha kupigia kura, kipaumbele kitatolewa kwa wagonjwa, watu wenye ulemavu, wazee, wajawazito na akina mama wanaonyonyesha watakaokwenda na watoto kituoni,” amesema.

Kuhusu wapiga kura kurudi nyumbani baada ya kupiga kura, Jaji Mwambegele amesema hilo ni sharti la kisheria na kwamba maadili ya uchaguzi yaliyosainiwa na kuridhiwa na vyama vyote vya siasa, Serikali na Tume yanaelekeza hivyo.

Alisisitiza kwa kusema “wapiga kura watatakiwa kuondoka kituoni mara wanapomaliza kupiga kura ili kuepusha msongamano na vitendo vinavyoweza kuchochea uvunjifu wa amani. Hivyo, Tume inawashauri wananchi kujiepusha na mikusanyiko katika maeneo ya vituo vya kupigia kura”.

Ametoa rai kwa wapiga kura katika Jimbo la Mbarali na kata sita zinazohusika na uchaguzi huu mdogo, kujitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura, ili kuwachagua viongozi wanaowataka.

Jumla ya vyama 17 vya siasa vinashiriki kwenye uchaguzi huo mdogo, vyama hivyo vinajumuisha AAFP, ACT–WAZALENDO, ADA–TADEA, ADC, CCK, CCM, CUF, Demokrasia Makini, DP, NLD, NRA, SAU, TLP, UDP, UMD, UPDP na NCCR–MAGEUZI.

Habari Mpya

  • Tume yatangaza matokeo ya Uchaguzi Jimbo la Mbarali na Kata Sita za Tanzania Bara
    September 21, 2023
  • ?Mwenyekiti wa Tume Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele atembelea na kukagua Uchaguzi Mdogo Jimbo la Mbarali
    September 19, 2023
  • Wapiga kura 216,282 kupiga kura uchaguzi mdogo wa Mbarali na kata sita
    September 19, 2023

Nifanyaje?

  • Kujiandikisha Kupiga Kura
  • Kupiga Kura

Machapisho

  • Jarida la Uchaguzi, Agosti, 2023
  • Jarida la Uchaguzi Toleo la Julai, 2023
  • Jarida la Uchaguzi Toleo la Machi, 2023
  • Jarida la Uchaguzi Toleo la Februari, 2023
  • Jarida la Uchaguzi Toleo la Januari, 2023
Tanzania Census 2022

Mawasiliano yetu

  • Address : P.O.Box 358, Dodoma, The National Electoral Commission, 5 Uchaguzi Road, 41107 Njedengwa Uchaguzi House
  • Namba ya Simu : +255 26 2962345-8
  • Nukushi : +255 26 2962348
  • Barua Pepe : uchaguzi@nec.go.tz
  • Tovuti : www.nec.go.tz

Linki za Haraka

  • Maktaba ya Tume.
  • Majukumu ya Msingi

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Bunge la Tanzania
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Msajili wa Vyama vya Siasa

Kuwa karibu nasi

Jiunge na orodha ya baruapepe zetu ili uhabarishwe na kupata notisi kuhusu taarifa zetu mpya

Tufuatilie

@2023 Tume ya Taifa ya Uchaguzi . Haki zote zimehifadhiwa

  • Ramani ya Tovuti
  • Wasiliana Nasi