Vyama 16 vyachukua Fomu za Uteuzi kugombea Ubunge Jimbo la Ushetu mkao wa Shinyanga
Imewekwa: September 18, 2021Vyama 16 vya siasa vimejitokeza kuchukua fomu za uteuzi kugombea kiti cha Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Ushetu Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Mkoa wa Shinyanga unaotarajiwa kufanyika tarehe 9 Oktoba mwaka 2021.
Vyama
vilivyojitokeza kuchukua fomu za uteuzi hadi kufikia tarehe 18 Septemba mwaka 2021
saa 10:00 jioni ni Chama cha DP, Chama cha CHAUMMA, NRA, ADC, AAFP, Sauti ya
Umma (SAU),
Vyama vingine
vilivyochukua fomu ni Cha cha ADA TADEA, UPDP, TLP, Demokrasia Makini, UMD,
NLD, UDP, CCK, CCM na Chama cha ACT Wazalendo.
NEC Habari imeshuhudia
baadhi ya wagombea wakichukua fomu za uteuzi huku kikuwepo na ushindani kati ya
wanawake na wanaume ambapo kati ya vyama 16 vilivyochukua fomu, vyama nane (8) vimewakilishwa
na wanawake.
Vyama
vilivyoteua wawakilishi wanawake kuchukua fomu za uteuzi ni Chama cha ADC, AAFP,
SAU, ADA-TADEA, UPDP, UMD, NLD na Chama cha CCK.
Msimamizi wa
Uchaguzi Jimbo la Ushetu Bw. Linno Pius Mwageni amesema fomu za uteuzi kwa
wagombea wa kiti cha Ubunge wa Jimbo hilo zimeanza kutolewa tarehe 13 hadi tarehe
19 kesho Jumalipi itakuwa ni siku ya Uteuzi wa wagombea.
Kwa upande
wake Msimamizi Msaidizi wa Jimbo la
Ushetu Godfrey Samwel Lwambura amewataka wagombea hao kuhakikisha wanajaza fumo
za uteuzi kwa usahihi na siku watakaporejesha fomu hizo watajaza Fomu Namba 10
ya kuheshimu Maadili ya Uchaguzi.
Kwa mujibu
wa ratiba ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Ushetu iliyotolewa na Tume ya
Taifa ya Uchaguzi, Kampeni za Uchaguzi zitaanza tarehe 20 Septemba, 2021 hadi
tarehe 8 Oktoba, 2021 na Siku ya Kupiga Kura itakua tarehe 9 Oktoba mwaka 2021.