Vyama 13 vya siasa vyateuliwa kugombea Ubunge Jimbo la Mbarali katika uchaguzi mdogo
Imewekwa: August 21, 2023.jpg)
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbarali Mkoani Mbeya Bw. Missana Kwangura amefanya uteuzi wa wagombea kutoka vyama 13 vya siasa kuwania kiti cha Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Mbarali unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Septemba mwaka 2023.
Wagombea walioteliwa na
vyama vyao ni Halima Abdalah Magambo (AAFP), Osward Joseph Mndeva (DP), Zavely
Raurent Seleleka (UDP), Exavery Town Mwataga (CCK), Morris Thomas Nkongolo
(TLP) na Modestus Dickson Kilufi (ACT Wazalendo).
Wengine ni Mary Moses
Daudi (UPDP), Fatuma Rashidi Ligania (NLD), Bahati Keneth Ndingo (CCM), Bariki
Oswald Mwanyalu (Demokrasia Makini), Hashim Abasi Mdemu (ADC), Mwajuma Noty
Mirambo (UMD), na Husseni Hasani Lusewa kutoka
Chama cha ADA- TADEA.
Baada ya uteuzi wa
wagombea Msimamizi wa Uchaguzi akabandika fomu za uteuzi kwenye eneo la wazi
kama inavyoekelezwa na sheria za uchaguzi ili kutoa fursa kwa vyama vya siasa,
wagombea na kukagua fomu hizo.
Akizungumza baada ya uteuzi Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mbarali Missana Kwangura amesema baada ya kukamilika kwa uteuzi wa wagombea, tarehe 20 Agosti mwaka 2023 kampeni za wagombea zitaanza rasmi hadi tarehe 18 Septemba mwaka 2023, hivyo amewataka wagombea na vyama vya siasa kufanya kampeni za kistaarabu.