Tume yawataka wanaokwenda kujiandikisha wawe na namba za simu ili kuendana na matakwa ya mashine za BVR
Imewekwa: July 28, 2019
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesisitiza kuwa Watanzania wanaokwenda kuandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wawe na nanmba za simu za mkononi kwani mashine ya BVR hairuhusu kumuandisha mwananchi bila kuweka namba ya simu.
Hayo yamesemwa na Mjumbe
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri wakati akitoa
elimu ya mpiga kura kupitia redio ya Victoria FM ya Bunda mkoani Mara.
Balozi Mapuri alisema
kila anayekwenda kuandikishwa aende akiwa na namba ya simu kwa sababu bila ya
kujaza namba ya simu mashine za BVR haziruhusu uandikishaji uendelee.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura unaendelea katika mikoa ya Manyara na Simu na katika halmashauri nne za mkoa wa Mara kuanzia
Julai 31 hadi Agosti 6 mwaka huu.
Halmashauri hizo ni Halmashauri ya Wilaya ya
Bunda, Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na Halmashauri
ya Mji wa Bunda.