Tume yatwaa Kombe Mchezo wa Kuvuta Kamba kwenye Bonanza la Ukaguzi
Imewekwa: March 20, 2023TIMU ya Kamba ya Tume ya Aifa ya Uchaguzi (NEC) imefanikiwa kutwaa kombe katika Bonanza la Ukaguzi lililofanyika Jijini Dodoma na kushirikisha timu zaidi ya sita.
NEC ilitwaa
ushindi huo baada ya kuwavuta kwa mivuto miwili Timu ya Ukaguzi.
Katika Mpira
wa Miguu NEC hawakufurukuta mbele ya Makao Makuu Jogging baada ya kuwatupa nje
kwa mikwaju ya penati ambao badae katika fainali walikutana Ugakuzi na Makao
Makuu na Makao Makuu kutwaa ubingwa wa Soka.
Katika mchezo
wa Mpira wa Netball timu ya Ukaguzi iliibuka kidedea baada ya kuwatndika bila
huruma timu za Wizara ya Afya na Madini.
Mapema
akizungumza wakati wa ufunguzi wa bonanza hilo, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG), Charles Kichere ametoa rai kwa watumishi wa umma wakiwemo wa Ofisi
yake kushiri kwenye michezo kwani ni tiba isiyo na gharama.
Taasisi
zilizoshiriki mbali na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Mfuko wa
Bima ya Afya ya Uchaguzi(NHIF), Wakala wa Barabara(Tanroads) Ofisi ya Rais
Ikulu na Wizara ya Afya.
Alisema ili
kuwa na afya njema ni vyema watumishi wakashiriki mazoezi na kusisitiza kuwa
mazoezi ni tiba isiyo na gharama kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza na pia
kuipunguzia Serikali mzigo wa kuhudumia magonjwa hayo.
"Kazi
zetu sisi Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali tunatumia muda mwingi kuandika
taarifa hivyo tumekuwa tukiweka utaratibu wa kutoka nje kufanya mazoezi na ni
utaratibu mzuri katika kulinda afya za watumishi."
Kichere pia
alisema wanatumia bonanza hilo kujiandaa tayari na bonazan lingine litakalokutanisha
na wabunge.
"
Wabunge ni watu ambao tunafanya kazi nao kwa karibu, hivyo mwezi ujao tutakuwa
na bonanza la kushirikiana na wabunge kwa hiyo hii ni sehemu ya mazoezi
yetu."
Kichere
alisema katika bonanza Hilo pia watalitumia kuchagia damu benki ya Taifa ya
damu Ili kusaidia kutoka maisha ya watu wanaohitaji damu.
Naye
Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya CAG,
Novat Mfalamagoha kutokana na mtindo wa maisha ya mwanadamu mazoezi ni mabadala
mzuri wa dawa za hospitali.
Pia alishauri wazazi kujenga tabia ya kuwashirikisha watoto kwenye mazoezi ambayo itawafanya kujenga moyo wa kupenda mazoezi.