Tume yatoa uamuzi wa rufaa 60 za wagombea ubunge na udiwani na kuwarejesha wagombea 34 wa udiwani kwenye uchaguzi
Imewekwa: September 11, 2020Tume ya Taifa ya Uchaguzi imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 60 kati ya hizo rufaa 2 ni za wagombea ubunge na 58 ni za wagombea udiwani katika kikao chake cha jana tarehe 10 Septemba 2020.
Hayo
yamesemwa jijini Dar es Salaam leo tarehe 11 Septemba, 2020 na Mkurugenzi wa
Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles kufuatia kukamilika
kwa uamuzi dhidi ya rufaa hizo.
Dkt.
Charles amesema Tume katika rufaa hizo imekubali rufaa moja na kumrejesha mgombea katika orodha ya wagombea kutoka kwenye
Jimbo la Iramba Magharibi na kukataa rufaa moja
ya mgombea ambaye uteuzi wake ulitenguliwa kutoka kwenye Jimbo la Iramba
Magharibi.
Amesema
Tume imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 58 za madiwani na kukubali rufaa 34 na kuwarejesha wagombea katika orodha ya wagombea udiwani.
Amezitaja
kata ambazo wagombea wake wamerejeshwa kuwa ni Kata za Kahororo (Bukoba),
Ishozi (Nkenge),Chongoleani (Tanga Jiji), Kirare (Tanga Jiji), Mwamanga (Magu),
Ng’haya (Magu), Riroda (Babati Vijini), Maswa Magharibi (Maswa), Kirumba
(Ilemela), na kata ya Bonga (Babati Vijini).
Kata
nyingine ni Kamagambo (Karagwe), Namelock (Kiteto), Masewa (Bariadi),
Bweranyange (Karagwe), Kituntu (Karagwe), Kamagambo (Karagwe), Msowero
(Kilosa), Lubugu (Magu), Lingeta (Meatu), Ifakara (Kilombero), Kiloli
(Sikonge), Mkoma (Rorya), na kata ya Nyamhongolo (Ilemela)
Dkt.
Charles amezitaja kata nyingine kuwa ni kata ya Sikonge (Sikonge), Tanganyika
(Muheza), Uhenga (Wanging’ombe), Babati (Babati), Vwawa (Mbozi), Lukanga
(Mkuranga), Langai (Simanjiro), Lutale (Magu), Majohe (Ilala), Namabengo
(Namtumbo) na Viwanja Sitini (Kilombero).
Katika
hatua nyingine, Dkt. Charles amesema pia Tume imekataa rufaa 23 za wagombea ambao hawakuteuliwa
kutoka kwenye Kata za Ilemela (Ilemela), Kayenze (Mwanza Jiji), Kiarare (Tanga
Jiji), Mabawa (Tanga Jiji), Ilemela (Ilemela), Kadoto (Maswa Magharibi), na
kata ya Iyela (Mbeya Jiji).
Kata
nyingine ambazo wagombea wake rufaa zao zimekataliwa ni kata ya Kirua Vunjo
Magharibi (Vunjo), Mji Mpya (Morogoro Mjini), Pugu (Ukonga), Tembela (Mbeya
Mji), Vikumburu (Kisarawe), Mecco (Ilemela), Kibara (Mwibara), Kiloleli
(Sikonge), Changarawe (Mafinga Mji), Igawilo (Mbeya Mjini), Msonga (Mkuranga),
Uru Kaskazini (Moshi Vijini), Kivukoni (Ilala), Maanga (Mbeya Mjini), Nsalaga
(Mbeya Mjini) na Jangwani (Ilala).
“Tume
pia imekataa rufaa 1 ya kupinga
walioteuliwa. Rufaa hiyo ni kutoka kwenye Kata ya Arri (Babati Vijijini).Idadi hii inafanya
jumla ya rufaa za wagombea Ubunge zilizofanyiwa uamuzi na Tume kufikia 113 na za wagombea Udiwani 103”, amesema Dkt. Charles.
Amesema
Tume itaendelea kutoa matokeo baada ya
usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku na kwamba wahusika wa rufaa hizo watajulishwa
kwa barua juu ya uamuzi wa Tume.