Tume yatoa uamuzi wa rufaa 46 za wagombea udiwani na kuwarejesha wagombea 24 kwenye uchaguzi
Imewekwa: September 12, 2020Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imezipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 46 za wagombea udiwani waliowasilisha rufaa zao Tume kutoka kata mbalimbali nchini.
Akitoa
taarifa kwa umma jijini Dar es Salaam leo tarehe 12 Septemba, 2020 Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa NEC Dkt. Wilson Mahera Charles amesema kati ya rufaa hizo Tume
imekubali rufaa 24 na kuwarejesha wagombea katika orodha ya wagombea Udiwani.
Ametaja
kata ambazo wagombea wake wamerejeshwa kuwa ni kata ya Dunda (Bagamoyo),
Mtwivila (Iringa Mjini), Kikilo (Kondoa), Makurumla (Ubungo), Hezya (Vwawa),
Makorongoni (Iringa Mjini), Bwawani (Arumeru Magharibi), Jinjimili (Magu),
Kimnyaki (Arumeru Magharibi).
Dkt.
Charles ametaja kata nyingine kuwa ni kata ya Lemanyata (Arumeru Magharibi),
Mkwawa (Iringa Mjini), Kisarawe II (Kigamboni), Makurumla (Ubungo), Mbabala
(Dodoma Mjini), Mpanda Hotel (Mpanda Mjini), Lusungo (Kyela), Same (Same),
Maisaka (Babati Mjini), Makuburi (Ubungo), Kibada (Kigamboni), Maore (Same
Mjini) na rufaa tatu kutoka Kata ya Mshindo (Iringa Mjini).
Katika
hatua nyingine, Dkt. Charles amesema Tume imekataa rufaa 13 za wagombea ambao
hawakuteuliwa kutoka kwenye Kata za Kawajense (Mpanda), Mjini Chirombola
(Ulanga), Mabokweni (Tanga Mjini).
Amezitaja
kata nyingine kuwa ni Chanika (Karagwe), Mwamala (Manonga), Kiomboi (Iramba
Magharibi), Mwasenkwa (Mbeya Mjini), Old Iramba (Iramba Magharibi), Magara
(Babati Vijijini), Arri (Babati Vijijini), Chapwa (Tunduma) na rufaa mbili
kutoka Kata ya Kibamba (Kibamba).
“Tume imekataa rufaa 9 za kupinga walioteuliwa
kutoka kwenye Kata za Nonde (Mbeya Mjini), Mwagata (Iringa Mjini), Mabibo
(Ubungo), Mkimbizi (Iringa Mjini), Kipanga (Sikonge), Nsoho (Mbeya Mjini),
Ilemi (Mbeya Mjini), Bagara (Babati Vijijini) na Nkinga (Manonga)”, amesema
Dkt. Charles.
Amesema
idadi hiyo ya rufaa 46 inafanya jumla ya rufaa za wagombea Ubunge zilizofanyiwa
uamuzi na Tume kufikia 113 na za wagombea Udiwani 149.
Tume
itaendelea kutoa matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku
na kwamba wahusika wa rufaa hizo watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa Tume.