Tume yashiriki Maonyesho ya Sabasaba ili kuelimisha Wapiga Kura
Imewekwa: August 28, 2017
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inashiriki katika maonyesho ya SabaSaba ili kuwapa fursa Wapiga Kura na Wananchi kwa ujumla kupata Elimu ya Mpiga Kura sambamba na kutoa maoni yao yatakayowezesha kuboresha Chaguzi zijazo.
Ushiriki wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi katika maonyesho ya SabaSaba ya Mwaka huu ni wa Kwanza tangu
kuanzishwa kwake miaka ishirini
iliyopita.
Lengo kuu la ushiriki huo wa NEC ni kuwawezesha Wananchi
kutoa maoni na Kero zao ikiwa ni pamoja
na kupata Elimu na Uelewa juu ya namna
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inavyotekeleza majukumu yake ambayo imepewa kwa
mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Naibu Katibu Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura
Bi.Givenes Aswile amewaomba wananchi kutembelea banda la Tume ya Taifa ya
Uchaguzi ambalo lipo katika Banda la Jakaya Kikwete kujifunza taratibu
mbalimbali za Uchaguzi .
Pia amewaomba wale wote watakaopata fursa ya kufika katika
banda la Tume kuwa huru kutoa maoni na ushauri wao wa jinsi ya kuboresha
utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na hata kama wana malalamiko yoyote
wayaainishe ili Tume iweze kuyapitia na kuyatafutia ufumbuzi .