Tume yapokea ujumbe kutoka Taasisi ya Tume za Uchaguzi Duniani (AWEB)
Imewekwa: December 14, 2017Ujumbe huo umekuja kujifunza kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) juu ya masuala mbalimbali ya uendeshaji Uchaguzi nchini ikiwemo matumizi ya vifaa vya kuandikishia wapiga kura.
Mkurugenzi wa Mipango na Oparesheni Bw. Lee Ju-Hwan alisema kuwa yeye na ujumbe wake wamekuja kubadilishana uzoefu katika technolojia ya Kuandikisha Wapiga Kura.
Ujumbe huo umekutana na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani na kufanya mazungumzo naye ofisini kwake baada ya kukutana na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya tume hiyo kutembelea ofisi mbalimbali za Tume hiyo na kujifunza.
Wakiwa katika kikao na baadhi ya Watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ujumbe huo wa watu watatu ulijifunza namna mashine ya Biometric Voter Registration (BVR) inavyofanya kazi na jinsi NEC ilivyoweza kuandikisha Wapiga Kura wengi kwa kutumia mashine technolojia hiyo na changamoto zake.
Aidha ujumbe huo umekuja na aina mpya ya technologia ambayo inauwezo wa kuandikisha Wapiga Kura, kutuma taarifa za Wapiga katika kanzidata kutoka katika kituo cha kujiandikishia na kuhakiki Wapiga Kura siku ya Uchaguzi .
Mashine hiyo ambayo ni ndogo ukilinganisha na ile BVR ina uwezo wa kutumiwa na mtu mmoja ambaye ataweza kumuandikisha Mpiga Kura katika hatua zote hadi kupata kitambulisho cha mpiga Kura na inabebeka kirahisi.
Ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi wa Mipango na Operesheni Lee Ju-Hwan, Mtafiti Moon Jueun na Mtaalamu wa Uchaguzi Park Jae Sumg.
Technologia hiyo mpya inaweza kurahisisha utendaji kazi katika masuala ya uandikishaji wapiga Kura, kuhakiki wapiga kura na kutuma taarifa katika kanzi dara.