• English
  • |
  • Maswali yaulizwayo Mara kwa Mara   |  
  • Staff Mail

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Uchaguzi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Wajumbe wa Tume
    • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Jinsi NEC Ilivyoanzishwa
  • Uchaguzi
    • Mifumo ya Uchaguzi
    • Mzunguko wa Uchaguzi
    • Uchaguzi Mkuu
    • Uchaguzi Mdogo
    • Matokeo ya Uchaguzi Mkuu
  • Machapisho
    • Sheria za Uchaguzi
    • Ripoti
    • Kanuni za Uchaguzi
    • Maadili ya Uchaguzi
    • Rufaa za Uchaguzi Mdogo 2021
    • Miongozo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020
    • Orodha ya Matokeo ya Rufaa za Ubunge zilizoamuliwa na Tume
    • Wagombea waliopita bila kupingwa
    • Wagombea katika Uchaguzi Mkuu 2020
    • Wabunge na Madiwani Wateule wa Viti Maalum Uchaguzi Mkuu 2020
    • Jarida la Tume kuhusu Uchaguzi Mkuu 2020
    • Mpango Mkakati wa NEC 2021/2022 – 2025/2026
    • Kura ya Maoni
    • Maelekezo
    • Orodha ya Majimbo na Kata
  • Wapiga Kura
    • Elimu ya Mpiga Kura
    • Takwimu za Wapiga Kura
    • Vituo vya Uandikishaji
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • NEC Online TV
    • Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Ratiba ya Kampeni za Wagombea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020
    • Voters Interaction System
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida la Tume la Uchaguzi Mkuu 2020
  • Zabuni/Mnada
    • Zabuni za Ndani
    • Zabuni za Kimataifa
  • Mawasiliano

Tume yapitia rufaa tatu na kuamua kuwarejesha wagombea udiwani katika Uchaguzi Mdogo wa Desemba 17, 2022

Imewekwa: December 07, 2022

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepitia, kuchambua na kufanya uamuzi wa rufaa tatu na kuwarejesha wagombea Udiwani katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge na Udiwani unaotarajia kufanyika tarehe 17 Desemba mwaka 2022.

Uamuzi huo umefanywa na kikao cha Tume kilichokaa tarehe 6 Desemba, 2022 baa da ya kupitia rufaa za wagombea Udiwani zilizowasilishwa kufuatia baadhi ya wagombea Udiwani kutoridhika na maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya kikao hicho iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera Charles, wagombea hao waliwasilisha rufaa Tume kufuatia pingamizi walizowasilisha baada ya uteuzi wa tarehe 30 Novemba, 2022 katika Kata 12 za Tanzania Bara.

Dkt. Charles alisema Tume imekubali rufaa ya Ndugu Joseph Yunja Machiya kupitia ACT-WAZALENDO na kumrejesha katika orodha ya wagombea wa Udiwani katika Kata ya Mwamalili, Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

“Tume imekubali rufaa ya Ndugu Vitali Mathias Maembe kupitia ACT-WAZALENDO na kumrejesha katika orodha ya wagombea wa Udiwani katika Kata ya Dunda, Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.” alisema Dkt. Charles na kuongeza kuwa:

“Tume imekubali rufaa ya Ndugu Samwel Azaria Mnyellah kupitia NCCR-MAGEUZI na kumrejesha katika orodha ya wagombea wa Udiwani katika Kata ya Majohe, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.”

Alifafanua kuwa Tume imefikia maamuzi hayo kwa kuzingatia Kifungu cha 44 (5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 kikisomwa pamoja na kanuni ya 29(1), (2) na 30 (4) za Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani), 2020.

Alibainisha kuwa vifungu hivyo vinatoa fursa kwa wagombea Udiwani kukata rufaa wanapokuwa hawajaridhika na uamuzi wa Wasimamizi wa Uchaguzi kutokana na pingamizi zilizowasilishwa na vinaipa Tume mamlaka ya kukubali au kutengua uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi.

Baada ya kuwarejesha wagombea hao, Dkt. Charles alieleza kuwa Tume imewapongeza wagombea na vyama vyao vya siasa ambao walifuata taratibu za kisheria katika kudai haki zao, kuhakikisha wanatimiza malengo yao ya kushiriki katika uchaguzi huu mdogo ili kupata ridhaa ya wananchi na kuwa viongozi katika kata husika.

“Aidha Tume inaendelea kuwakumbusha wadau wote wa uchaguzi kuzingatia na kufuata njia sahihi zilizowekwa kisheria, ili kutatua changamoto zozote zinazojitokeza katika kipindi hiki cha kampeni kuelekea uchaguzi huu mdogo, ikiwemo kufuata maadili ya uchaguzi ambayo vyama vyote vya siasa viliridhia kuyafuata wakati wa uchaguzi.” alisema Dkt. Charles na kuongeza kuwa:

“Kwa upande mwingine Tume pia inawakumbusha wasimamizi na watendaji wote wa uchaguzi katika maeneo husika kuzingatia sheria, kanuni, taratibu, maelekezo ya Tume katika kuendesha na kusimamia uchaguzi huu.”

Alisema kutokana na uamuzi huo, Uchaguzi huu Mdogo wa Udiwani unafanyika katika kata Saba ambazo ni Majohe (Dar es Salaam CC) Dar es Salaam, Mndumbwe (Tandahimba DC) Mtwara, Njombe Mjini (Njombe TC) Njombe, Dunda (Bagamoyo DC) Pwani, Mwamalili (Shinyanga MC) Shinyanga, Mnyanjani (Tanga CC) Tanga, na Vibaoni (Handeni DC) Tanga.

Kata hizo saba zitaungana na Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Amani, Wilaya ya Mjini, Zanzibar utakaofanyika siku ya Jumamosi, tarehe 17 Disemba, 2022 ambapo Upigaji Kura utafanyika katika vituo vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Ili kufanikisha uchaguzi huo, Dkt. Mahera alisema Tume inatoa rai kwa wananchi wote wa maeneo hayo kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.

Habari Mpya

  • Tume yashiriki Maonesho ya Sherehe za Miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar
    January 02, 2023
  • Wapiga Kura 114,647 walioandikishwa kushiriki Uchaguzi Mdogo Jimbo la Amani na Kata Saba
    December 16, 2022
  • Wapiga Kura 114,647 walioandikishwa kushiriki Uchaguzi Mdogo Jimbo la Amani na Kata Sita za Tanzania Bara
    December 16, 2022

Nifanyaje?

  • Kujiandikisha Kupiga Kura
  • Kupiga Kura

Machapisho

  • Mpango Mkakati wa NEC 2021/22 – 2025/26
  • Taarifa ya Tathmini ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2020
  • Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa mwaka 2020
  • Wabunge Wanawake Walioteuliwa Viti Maalum Uchaguzi Mkuu 2020
Tanzania Census 2022

Mawasiliano yetu

  • Address : P.O.Box 358, Dodoma, The National Electoral Commission, 5 Uchaguzi Road, 41107 Njedengwa Uchaguzi House
  • Namba ya Simu : +255 26 2962345-8
  • Nukushi : +255 26 2962348
  • Barua Pepe : uchaguzi@nec.go.tz
  • Tovuti : www.nec.go.tz

Linki za Haraka

  • Maktaba ya Tume.
  • Majukumu ya Msingi

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Bunge la Tanzania
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Msajili wa Vyama vya Siasa

Kuwa karibu nasi

Jiunge na orodha ya baruapepe zetu ili uhabarishwe na kupata notisi kuhusu taarifa zetu mpya

Tufuatilie

@2023 Tume ya Taifa ya Uchaguzi . Haki zote zimehifadhiwa

  • Ramani ya Tovuti
  • Wasiliana Nasi