Tume yakutana na Wakala wa Majenge kuzungumzia Ujenzi wa Jengo Dodoma
Imewekwa: August 28, 2017
Mtendaji Mkuu Wakala wa Majengo Nchini (TBA) Bwana Elius Mwakalinga ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuendesha Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 kwa mafanikio makubwa na kuivusha nchi kwa Salama na Amani.
Bwana Mwakalinga amesema hayo katika kikao na Menejimenti ya Tume ya Taifa
ya Uchaguzi kilichofanyika katika ukumbi wa Tume jijini Dar es Salaam
14.07.2016 kujadili maandalizi ya ujenzi wa Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi
huko Mkoani Dodoma.
Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima
Ramadhani ameieleza TBA historia ya Tume, hali ilivyo sasa na mahitaji mapya
katika jengo linalotarajiwa kujengwa huko Dodoma katika eneo la Njendengwa
Block D.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa sasa imepanga katika jengo la Posta Makao
Makuu mazingira ambayo siyo rafiki kwa utendaji wa kazi za Tume hasa wakati wa kipindi
cha Uchaguzi Mkuu kutokana na unyeti wa kazi zinazofanywa na Tume,hasa kwa kuwa
uchaguzi uhusisha maslahi ya watu wengi na Jengo hilo la Posta kuwa na
Wapangaji binafsi.
Mwezi Mei Mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe
Magufuli aliipatia Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kiasi cha Tsh.Bil.12 kwa ajili ya
kujenga jengo la ofisi kwa sharti la kujenga ofisi hizo huko Dodoma.
Kufuatia Uamuzi huo,Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Mjini Dodoma (CDA), iliipatia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Jengo hilo chenye ukubwa wa mita za mraba 36,000 ili liweze kutumika kwa kazi hiyo.