Tume yafanya uamuzi wa rufaa 87 za wagombea udiwani na kuwerejesha wagombea 47 wa udiwani
Imewekwa: September 15, 2020Tume ya Taifa ya Uchaguzi imezipitia, imechambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 87za wagombea udiwani na kuwarejesha wagombea 47 wa udiwani na kuwarejesha wagombea udiwani katika orodha ya wagombea udiwani.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Dkt. Wilson Mahera Charles wakati
akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu uamuzi wa kikao cha Tume kilichokaa
jana jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Charles ametaja kata ambazo wagombea wake wamerejeshwa kuwa ni kata ya Mwanhuzi
(Meatu), Kondoa Mjini (Kondoa Mjini) Msasa (Handeni Mjini), Bunju (Kawe), Bunju
(Kawe), Ipagala (Dodoma Mjini), Isuto (Mbeya Vijijini), Iwiji (Mbeya Vijijini),
Kichangani (Morogoro Mjini), Kimara (Ubungo).
Ametaja
kata nyingine kuwa ni kata ya Likongowele (Liwale), Matumbulu (Dodoma Mjini),
Nsalala (Mbeya Vijijini), Ulenje (Mbeya Vijijini), Muriti (Ukerewe), Ruvu (Same Magharibi), Kisutu (Bagamoyo),
Majimaji (Tunduru), Mtibwa (Mvomero), Unyianga (Singida Mjini) na Kagondo
(Bukoba Mjini).
Wagombea
wengine waliorejeshwa ni kutokea kwenye kata ya Kaloleni (Moshi Mjini), Mlabani
(Kilombero), Fukayosi (Bagamoyo), Igurwa (Karagwe), Kauzeni (Morogoro Mjini),
Maisaka (Babati Mjini), Ndama (Karagwe) Olorien/Magaiduru (Ngorongoro), Kilole
(Lushoto), Ngwelo (Lushoto), Hondomairo (Kondoa Mjini), Nyasiura (Bunda Mjini), Ikhanoda (Singida
Kaskazini), Nyabiyonza (Karagwe), Kibiti (Kibiti), Ruvu Remit (Simanjiro), Ihanda (Karagwe),
Mabanda (Handeni Mjini), Bungu (Kibiti), Kapala Msenga (Mpanda Vijijini),
Businde (Kyerwa), Igoma (Mbeya Vijijini), Likongowele (Liwale), Shizuvi (Mbeya
Vijijini), Mlembwe (Liwale) na Tambukareli (Dodoma Mjini).
Katika
hatua nyingine, Dkt. Charles amesema Tume pia imekataa rufaa 30 za wagombea udiwani ambao
hawakuteuliwa kutoka kwenye kata za Tongwe (Muheza) Kiomboi (Iramba Magharibi),
Jangwani (Ilala), Mlali (Mvomero), Kiloleni (Sikonge), Mbasa (Kilombero),
Dakawa (Mvomero),
“Kata
nyingine ni Dakawa (Mvomero), Jibondo (Mafia), Kigombe (Muheza), Buhumbi (Magu),
Mlali (Mvomero), Olbalbal (Ngorongoro), Kidete (Kilosa), Bugene (Karagwe),
Kihanga (Karagwe), Mabogini (Moshi Vijijini), Hemtoye (Mlalo), Mlali (Mvomero),
Mbaramo (Mlalo), Mbaru (Mlalo), Okaoni (Moshi Vijijini), Nangando (Liwale),
Magomeni (Kinondoni), Kitangiri (Ilemela),
Dareda (Babati Vijijini), Iganjo (Mbeya Mjini), Ipembe (Singida Mjini), Kilema
Kaskazini (Vunjo) na Nyamhongolo (Ilemela)”, amesema Dkt. Charles.
Dkt.
Charles ameongeza kuwa, Tume imekataa rufaa
10 za kupinga wagombea udiwani walioteuliwa kutoka kata za Forest (Mbeya
Mjini), Mabatini (Mbeya Mjini), Mkowe (Kalambo), Kaloleni (Moshi Mjini),
Mwangoi (Mlalo), Malibwi (Lushoto), Kwa Kilosa (Iringa Mjini), Kihesa (Iringa
Mjini), Nzubuka (Tabora Kaskazini) na Ihumwa (Dodoma Mjini).
Amesema
idadi hiyo inafanya jumla ya rufaa za wagombea Udiwani zilizotolewa uamuzi
kufikia 331 na Tume itaendelea kutoa
matokeo baada ya usajili na uchambuzi wa rufaa hizo kila siku.
Ameongeza
kuwa wahusika wa rufaa hizo watajulishwa kwa barua juu ya uamuzi wa Tume.