Tume ya Taifa ya Uchaguzi yapata Mwenyekiti Mpya
Imewekwa: December 14, 2017Mhe. Jaji Semistocles Kaijage ameteuliwa kuongoza Tume kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016 akichukua nafasi ya Mhe. Jaji Mstaafu Damiani Lubuva ambaye muda wake wa kuwa Mwenyekiti umemalizika rasmi mnamo tarehe 19 Desemba, 2016.
Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemteua Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mahamoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kipindi kingine cha miaka mitano kuanzia tarehe 20 Desemba, 2016.
Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mahamoud Hamid alikuwa Makamu Mwenyekiti wa NEC na aliyemaliza kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano mnamo tarehe 19 Desemba, 2016.