Tume kuanza Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuanzia Julai, 2019
Imewekwa: June 13, 2019Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itaboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, awamu
ya kwanza kuanzia mwezi Julai, 2019 kwa kutumia Teknolojia ya kieletroniki ya
Biometriki (BVR).
Hayo
yalisemwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Mahakama ya
Rufaa), Semistocles Kaijage wakati alipokutana na wakilishi wa Vyama vya Siasa
vilivyopata Usajili wa Kudumu katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere
International Convention Centre (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti,
Jaji Semistocles Kaijage alisema kulingana na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,
Kifungu cha 21 (5), sura 343 na Sheria
ya Uchaguzi ya Serikali ya Mitaa
Sura ya 292 Tume inapaswa
kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mara mbili katika Uchaguzi Mkuu
mmoja na Uchaguzi Mkuu mwingine unaofuata.
Uboreshaji
wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili utafanyika baada ya
kukamilika kwa uboreshaji awamu ya kwanza.
Mhe,
Jaji Kaijage alisema kuwa uboreshaji huo unafanyika baada ya kukamilika kwa
sehemu kubwa ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari kama uhakiki wa vituo vya
kandikisha Wapiga Kura, uandikishaji wa majaribio wa Wapiga Kura katika Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura, maandalizi ya vifaa vya Uboreshaji wa Daftari na
mkakati wa Elimu ya Mpiga Kura.
Mwenyekiti
alisema kuwa uandikishaji wa Wapiga Kura wa mwaka huu, 2019 Tume itaandikisha
Wapiga Kura wapya na wale waliopoteza kadi za kupigia kura au kadi zao
kuharibika, wanaorekebisha taarifa zao na bila kusahau waliohama kutoka maeneo
yao ya awali na kuhamia maeneo mengine ya Uchaguzi tofauti na uandikishaji wa
mwaka 2015 ambapo wapiga kura wote nchi nzima waliandikishwa.
Ili
kuhamasisha wananchi wajitokeze kujiandikisha kwa wingi, Tume itatumia njia
mbalimbali za Elimu ya Mpiga Kura kuwaelimisha kupitia Taasisi au Asasi za
Kiraia zenye sifa ya kutoa elimu hiyo, kukutana na wananchi ana kwa ana kwa
kushiriki maonyesho mbalimbali, mikusanyiko ya kijamii, gari la matangazo la
Tume, Vyombo vya Habari, mitandao ya kijamii, Makala za magazeti na machapisho
mbalimbali kama mabango na vipeperushi.
Mwenyuekiti
pia aliwambia wawakilishi wa Vyama vya siasa kuleta majina ya mawakala wao Tume
siku saba kabla ya Uboreshaji ili waapishwe kupata vibali kwa ajili ya kusimamia
uandikishaji wa Wapiga Kura vituoni.
Mwaka
huu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itakuwa na vituo vya uandikishaji Wapiga
Kura 37, 407 tofauti na vituo 36,549 vilivyotumika mwaka 2015 na Tume ya
Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) itatumia vituo vya kuandikisha Wapiga Kura 407
tofauti na idadi ya vituo 380 vilivyotumika mwaka 2015.
Aidha,
Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dkt. Athumani J. Kihamia alisema kuwa maeneo
yanayokubalika kuwekwa vituoa vya uandikishaji Wapiga Kura kulingana na Kanuni
ya 12 (2) ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari chini ya Sheria ya Uchaguzi, Sura
ya 343 na Kamuni ya 12 (2) ya Kanuni ya Uboreshaji wa Daftari chini ya Sheria
ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292
ni majengo ya umma na maeneo ya
wazi yanayofikika kwa urahisi.
Pamoja
na hayo, Mkurugenzi wa Uchaguzi alibainisha maeneo yasiyokubalika kwa mujibu wa
Kanuni ya 12 (3) ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari ya Sheria ya Uchaguzi, Sura
ya 343 na Kanuni ya 15 (3) ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari chini ya Sheria
ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ni Kambi za Jeshi, Numba za Ibada
na Ofisi za Vyama vya Siasa