"Tume haikuagiza walipoteza kadi kudaiwa taarifa ya Polisi ya kupotelewa" Jaji Kaijage.
Imewekwa: July 28, 2019
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Semistocles Kaijage amesema Tume haijaagiza wapiga kura walipoteza kadi zao za kupigia kura kudaiwa taarifa ya upotevu (loss report) ili wapatiwe kadi mpya.
Hivyo amewataka
watendaji wa uandikishaji kwenye Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
kufuata maelekezo ya Tume yaliyotolewa kwao wakati wa mafunzo.
Jaji Kaijage ameyasema
hayo mjini Babati kufuatia taarifa za baadhi wananchi waliopotelewa na kadi zao
za kupigia kura kutakiwa kwenda na loss report ya Polisi ili wapatiwe kadi nyingine.
Aliagiza kuwa mpiga kura anatakiwa kutaja majina yake aliyotumia kujiandikishia mwaka 2015 kwa usahihi kwenye kituo alicho jiandikishia wakati huo ili apewe kadi mpya.