Rais ,Dkt. John Pombe Magufuli awaapisha Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume
Imewekwa: December 14, 2017
Pia Mhe. Rais amemwapisha Jaji mstaafu Hamid Mahmoud Hamid kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Mhe. Jaji Mstaafu Hamid Mahamoud Hamid alikuwa Makamu Mwenyekiti wa NEC aliyemaliza kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano Desemba 19, 2016.
Hafla ya kuwaapisha viongozi hao imefanyika Ikulu, jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Anjellah Kairuki, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju.
Akizungumza na vyombo vya Habari mara baada ya kuapishwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Semistocles Kaijage amesema kuwa katika kutekeleza majukumu yake atazingatia kiapo cha Uenyekiti alichokitoa, Katiba na Sheria zinazoongoza chaguzi mbalimbali nchini.