NIDA yapokea BVR kits 5000 kutoka NEC
Imewekwa: August 28, 2017
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa BVR kits hizo Meneja wa
mifumo na ukarabati kutoka NIDA Mohamed Mashaka amesema kukabidhiwa kwa vifaa
hivyo kumekuja wakati muafaka wakati mamlaka hiyo ikijipanga kuhakikisha
watanzania wengi wanapatiwa vitambulisho vya taifa.
Alibainisha kuwa kwa sasa NIDA ina Kits 1503 ambazo hazitoshi
ndiyo maana wameomba kuongezea BVR Kits 5,000 angalau ziwezekuongeza nguvu
zaidi katika zoezi la kuandikisha Vitambulisho vya Taifa.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Idara ya Daftari la Kudumu la
Wapiga Kura kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw.Amos Madaha
aliwahakikishia wawakilishi hao wa NIDA kwamba vifaa walivyowakabidhi vina
ubora wa hali ya juu ndio maana wakati wa uandikishaji wa wapiga Kura NEC
iliweza kuandikisha Wapiga Kura wengi kwa kipindi kifupi.
Kabla ya makabidhiano ya BVR hizo Mamlaka ya vitambulisho vya
Taoifa NIDA walikwishachukua BVR kits 6 kwaajili ya mafunzo kwa maafisa wao na
walishajifunza na kuzielewa tayari kwa kuanza zoezi la uandikishaji.
Wakati wa makabidhiano hayo baadhi ya taasisi za serikali zilituma wawakilishi wao kushuhudia zoezi hilo ambao ni kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Wizara ya fedha.