Mwaliko wa Taasisi na Asasi za kutoa Elimu ya Mpiga Kura Uchaguzi Mdogo Jimbo la Amani na Kata 12
Imewekwa: November 02, 2022
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inazialika Taasisi na Asasi za Kiraia kutuma maombi ya kibali cha kutoa Elimu ya Mpiga Kura katika Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Amani na Kata 12 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 17 Desemba, 2022. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 9 Novemba mwaka 2022 na Bofya hapa kuangalia Vigezo na Masharti ya maombi ya kibali.