Muundo wa Taasisi
MUUNDO WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
Tume inaundwa na Wajumbe saba (7),
miongoni mwao wakiwemo Mwenyekiti na
Makamu Mwenyekiti ambao wanapaswa kuwa
na sifa ya Jaji wa Mahakama Kuu au
Mahakama ya Rufani. Katika Uteuzi, Rais
anazingatia kuwa endapo Mwenyekiti ni
mtu anayetoka sehemu moja ya Muungano,
Makamu wake atakuwa ni mtu
anayetoka sehemu ya pili ya Muungano.
Hii, ni kwa mujibu wa Ibara ya 74(1) na (2)
ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977, na Kifungu cha
4(1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,
Sura ya 343.
Aidha, Mjumbe mmoja anateuliwa kutoka
miongoni mwa Wanachama wa Chama cha
Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law
Society - TLS) na Wajumbe wengine
wanne (4) wanatakiwa wawe na uelewa wa
kutosha kuhusiana na kusimamia na
kuendesha Uchaguzi wa Wabunge au sifa
nyingine kama ambavyo Rais wa Jamhuri
ya Muungano atakavyoona inafaa kwa ajili
ya kuendesha shughuli za Tume.
Tume ina jumla ya Wajumbe saba (7), kama inavyoonesha hapa chini:-
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Na. Jina Wadhifa
1. Mhe. Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele, Mwenyekiti
2. Mhe. Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk, Makamu Mweyekiti
3. Mhe. Jaji Asina Abdillah Omari, Mjumbe
4. Mhe. Balozi Omar Ramadhani Mapuri, Mjumbe
5. Mhe. Magdalena Kamugisha Rwebangira, Mjumbe
6. Mhe. Jaji Rufaa Mwanaisha Athuman Kwariko, Mjumbe
7. Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar, Mjumbe
Wajumbe wa Tume hukaa Madarakani kwa kipindi cha miaka mitano tangu
kuteuliwa kwao, lakini Rais anaweza
kuwateua tena kwa kipindi kingine kadri
atakavyoona inafaa.
Katika utekelezaji wa majukumu yake,
Tume husaidiwa na Sekretarieti
inayoongozwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi
ambaye ndiye Mtendaji Mkuu na Katibu
wa Tume. Kwa sasa Mkurugenzi wa Uchaguzi
ni Ndugu Kailima, R.K.
Aidha, Tume ina Idara 6, Ofisi ya Zanzibar na Vitengo 3 kama ifuatavyo:-
(i) Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi;
Bofya Majukumu ya Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi
(ii) Idara ya Daftari na TEHAMA;
Bofya Majukumu ya Idara ya Daftari na TEHAMA
(iii) Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura;
Bofya Majukumu ya Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura
(iv) Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu;
Bofya Majukumu ya Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
(v) Idara ya Mipango Ufuatiliaji na Tathmini;
Bofya Majukumu ya Idara ya Mipango Ufuatiliaji na Tathmini
(vi) Idara ya Usimamizi wa Manunuzi na Lojistiki;
Bofya Majukumu ya Idara ya Usimamizi wa Manunuzi na Lojistiki
(vii) Kitengo cha Huduma za Sheria
Bofya Majukumu ya Kitengo cha Huduma za Sheria
(viii) Ofisi ya Zanzibar;
Bofya Majukumu ya Ofisi ya Zanzibar
(ix) Kitengo cha Fedha na Uhasibu; na
Bofya Majukumu ya Kitengo cha Fedha na Uhasibu; na
(x) Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani;