• English
  • |
  • Maswali yaulizwayo Mara kwa Mara   |  
  • Staff Mail

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Uchaguzi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Wajumbe wa Tume
    • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Jinsi NEC Ilivyoanzishwa
  • Uchaguzi
    • Mifumo ya Uchaguzi
    • Mzunguko wa Uchaguzi
    • Uchaguzi Mkuu
    • Uchaguzi Mdogo
    • Matokeo ya Uchaguzi Mkuu
  • Machapisho
    • Sheria za Uchaguzi
    • Ripoti
    • Kanuni za Uchaguzi
    • Maadili ya Uchaguzi
    • Rufaa za Uchaguzi Mdogo 2021
    • Miongozo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020
    • Orodha ya Matokeo ya Rufaa za Ubunge zilizoamuliwa na Tume
    • Wagombea waliopita bila kupingwa
    • Wagombea katika Uchaguzi Mkuu 2020
    • Wabunge na Madiwani Wateule wa Viti Maalum Uchaguzi Mkuu 2020
    • Jarida la Tume kuhusu Uchaguzi Mkuu 2020
    • Mpango Mkakati wa NEC 2021/2022 – 2025/2026
    • Kura ya Maoni
    • Maelekezo
    • Orodha ya Majimbo na Kata
  • Wapiga Kura
    • Elimu ya Mpiga Kura
    • Takwimu za Wapiga Kura
    • Vituo vya Uandikishaji
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • NEC Online TV
    • Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Ratiba ya Kampeni za Wagombea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020
    • Voters Interaction System
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida la Tume la Uchaguzi Mkuu 2020
  • Zabuni/Mnada
    • Zabuni za Ndani
    • Zabuni za Kimataifa
  • Mawasiliano

Wapiga Kura 114,647 walioandikishwa kushiriki Uchaguzi Mdogo Jimbo la Amani na Kata Saba

Imewekwa: December 16, 2022

Wapiga Kura 114,647 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wanatarajiwa kushiriki katika uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Amani Mkoa wa Mjini, Zanzibar na Kata saba za Tanzania Bara tarehe 17 Desemba, 2022.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele katika Risala ya Uchaguzi huo mdogo unaotarajiwa kufanyika kesho tarehe 17 Desemba, 2022 na kusema kuwa vituo vituo 289 vya kupigia kura vitatumika.

“Tume imekamilisha maandalizi muhimu ikiwemo usambazaji wa vifaa vya uchaguzi na mafunzo kwa watendaji wa uchaguzi katika ngazi ya vituo vya kupigia kura” alisema Jaji wa Rufaa Mwambegele.

Jaji wa Rufaa Mwambelegele amesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewataka wasimamizi wa uchaguzi, vyama vya siasa na wagombea kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi wakati wa Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Amani, Mkoa wa Mjini, Zanzibar na Uchaguzi wa Udiwani katika Kata saba za Tanzania Bara.

Mbali na jimbo la Amani pia uchaguzi huo mdogo utashirikisha, Kata za Majohe (Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam), Mndumbwe (Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba), Njombe Mjini (Halmashauri ya Mji wa Njombe), Dunda (Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo), Mwamalili (Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga), Mnyanjani (Halmashauri ya Jiji la Tanga) na Vibaoni (Halmashauri ya Wilaya ya Handeni).

Aidha, amevitaka vyama vya siasa, wagombea na wadau wa uchaguzi kuepuka kujihusisha na matukio yenye viashiria vya uvunjifu wa amani kwani jukumu la kulinda amani ni la kila mwananchi, hivyo wahakikishe wanalinda amani iliyopo sasa kwenye jimbo na kata zinazofanya uchaguzi huo.

Jaji wa Rufaa Mwambegele amesema Sheria na Kanuni za Uchaguzi zimeweka mamlaka na taratibu zinazotakiwa kufuatwa iwapo kutakuwepo na malalamiko yoyote wakati wa uchaguzi, hivyo amevitaka vyama vya siasa na wagombea kufuata taratibu hizo ili kuuufanya uchaguzi huo ufanyike kwa uhuru na haki.

Mweyekiti huyo wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi amewataka wapiga kura wote waliojiandikisha katika jimbo ya Amani na Kata saba za Tanzania Bara kujitokeza kupiga kura ili waweze kuwachagua Mbunge na madiwani wanaowataka.

Amevitaka vyama vya siasa wagombea na wafuasi wao kuzingatia kuwa kampeni za uchaguzi zimekamilika tarehe 16 Desemba, 2022 saa 12:00 jioni hivyo hawaruhusiwi kufanya mikutano ya kampeni kuanzia muda huo na hawaruhusiwi kutumia alama za vyama zinazoashiria kampeni kama vile vipeperushi, bendera na mavazi.

Aidha Jaji Rufaa Mwambegele amevikumbusha vyama vya Siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi wa huo, kuzingatia wajibu wao wa kuweka mawakala katika vituo vyote vya kupigia, kuhesabu na kujumlishia kura.

“Pili upigaji kura utafanyika katika vituo vya kupigia kura vile vile vilivyotumika wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni.Iwapo watakuwepo wapiga kura katika mstari ambao walifika kabla ya saa 10:00 jioni na hawajapiga kura, wataruhusiwa kupiga kura, mtu yeyote hataruhusiwa kujiunga katika mstari wa wapiga kura baada ya saa 10:00 jioni”alisema Jaji Rufaa Mwambegele na kuongeza:

“Watakaoruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Amani Wilaya ya Mjini Zanzibar ni wale tu walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na wana kadi za mpiga kura” alisema Jaji wa Rufaa Mwambegele.

Aidha Jaji wa Rufaa Mwambegele alisema “Kwa upande wa uchaguzi mdogo wa madiwani watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wana kadi zao za mpiga kura. Hata hivyo, Tume kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 61(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 pamoja na kifungu cha 62(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Sura 292, imeruhusu wapiga kura ambao wamepoteza kadi zao au kadi kuharibika kutumia vitambulisho mbadala”.

Amevitaja vitambulisho mbadala kuwa ni Passi ya Kusafiria, Leseni ya Udereva au Kitambulisho cha Uraia kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Mpiga kura aliyepoteza kadi au kadi yake kuharibika ataruhusiwa kutumia kitambulisho mbadala iwapo tu atakuwa ameandikishwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na jina lake lipo kwenye orodha ya wapiga kura anapokwenda kupiga kura. Aidha majina yake yaliyopo katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura yafanane na yale yaliyopo katika kitambulisho mbadala.

Jaji wa Rufaa Mwambegele amekumbusha kuwa katika vituo vya kupigia kura kipaumbele kitatolewa kwa wagonjwa, watu wenye ulemavu, wazee, wajawazito na akina mama wanaonyonyesha watakaokuwa na watoto vituoni na kutakuwa na majalada ya nuktanundu katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa kuona ili weweze kupiga kura wenyewe.

Alifafanua kuwa kwa wapiga kura wenye ulemavu wa kuona ambao hawawezi kutumia majalada hayo wanaruhusiwa kwenda vituoni na watu watakaowachagua wenyewe kwa ajili ya kuwasaidia kupiga kura.

Amewakumbusha wapiga kura kuzingatia Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2020 yaliyokubaliwa na wahusika wote vikiwemo vyama vya siasa, kuwa wapiga kura watatakiwa kuondoka vituoni mara tu baada ya kupiga kura, hivyo Tume imewashauri wananchi kujiepusha na mikusanyiko katika maeneo ya vituo vya kupigia kura.

Jumla ya vyama vya siasa 16 vimesimamisha wagombea katika uchaguzi huo mdogo ambapo Tume imevipongeza vyama hivyo na wagombea wao kwa kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba kujitokeza kushiriki katika uchaguzi huu mdogo wa Ubunge na Udiwani.

Habari Mpya

  • Tume yatwaa Kombe Mchezo wa Kuvuta Kamba kwenye Bonanza la Ukaguzi
    March 20, 2023
  • Tume yashiriki Maonesho ya Sherehe za Miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar
    January 02, 2023
  • Wapiga Kura 114,647 walioandikishwa kushiriki Uchaguzi Mdogo Jimbo la Amani na Kata Saba
    December 16, 2022

Nifanyaje?

  • Kujiandikisha Kupiga Kura
  • Kupiga Kura

Machapisho

  • Mpango Mkakati wa NEC 2021/22 – 2025/26
  • Taarifa ya Tathmini ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2020
  • Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020
  • Matokeo ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa mwaka 2020
  • Wabunge Wanawake Walioteuliwa Viti Maalum Uchaguzi Mkuu 2020
Tanzania Census 2022

Mawasiliano yetu

  • Address : P.O.Box 358, Dodoma, The National Electoral Commission, 5 Uchaguzi Road, 41107 Njedengwa Uchaguzi House
  • Namba ya Simu : +255 26 2962345-8
  • Nukushi : +255 26 2962348
  • Barua Pepe : uchaguzi@nec.go.tz
  • Tovuti : www.nec.go.tz

Linki za Haraka

  • Maktaba ya Tume.
  • Majukumu ya Msingi

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Bunge la Tanzania
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Msajili wa Vyama vya Siasa

Kuwa karibu nasi

Jiunge na orodha ya baruapepe zetu ili uhabarishwe na kupata notisi kuhusu taarifa zetu mpya

Tufuatilie

@2023 Tume ya Taifa ya Uchaguzi . Haki zote zimehifadhiwa

  • Ramani ya Tovuti
  • Wasiliana Nasi