Ujumbe wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho wafanya ziara ya mafunzo Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Imewekwa: January 19, 2022
Ujumbe wa watu wa tatu kutoka Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho (IEF Lesotho) ukuingozwa na Mjumbe wa Tume hiyo,Dkt. Karabo Mokobocho Monlakoana upo nchini kwa ziara ya mafunzo ambapo wametembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dodoma.
Katika Ziara hiyo waliyoifanya katika Makao Makuu ya Tume,
ujumbe huo ulipokelewa na Mjumbe wa Tume, Asina Omar na Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Dkt. Wilson Mahera Charles na kisha kuwatembeza katika jengo hilo na kujionea shughuli
mbalimbali zinazofanywa na Tume ya Uchaguzi Tanzania.
Mjumbe huyo kutoka Tume ya Lesotho, IEF Lesotho Dkt Monlakoana
ameambatana na Maofisa kutoka Tume hiyo, Afisa Rasilimali watu, Thato Moete na
Meneja Msaidizi wa Fedha Azael Limpho Monese.
Aidha ujumbe huo ulipata fursa ya kuzungumza na menejimenti ya
Tume na baadae Mkurugenzi, Dkt Mahera akatoa wasilisho kuhusiana na Muundo,
majukumu na Kazi za Tume.