• English
  • |
  • Maswali yaulizwayo Mara kwa Mara   |  
  • Staff Mail

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Tume ya Taifa ya Uchaguzi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Wajumbe wa Tume
    • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Jinsi NEC Ilivyoanzishwa
  • Uchaguzi
    • Mifumo ya Uchaguzi
    • Mzunguko wa Uchaguzi
    • Uchaguzi Mkuu
    • Uchaguzi Mdogo
    • Matokeo ya Uchaguzi Mkuu
  • Machapisho
    • Sheria za Uchaguzi
    • Ripoti
    • Kanuni za Uchaguzi
    • Maadili ya Uchaguzi
    • Rufaa za Uchaguzi Mdogo 2021
    • Miongozo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020
    • Orodha ya Matokeo ya Rufaa za Ubunge zilizoamuliwa na Tume
    • Wagombea waliopita bila kupingwa
    • Wagombea katika Uchaguzi Mkuu 2020
    • Wabunge na Madiwani Wateule wa Viti Maalum Uchaguzi Mkuu 2020
    • Jarida la Tume kuhusu Uchaguzi Mkuu 2020
    • Mpango Mkakati wa NEC 2021/2022 – 2025/2026
    • Kura ya Maoni
    • Maelekezo
    • Orodha ya Majimbo na Kata
  • Wapiga Kura
    • Elimu ya Mpiga Kura
    • Takwimu za Wapiga Kura
    • Vituo vya Uandikishaji
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • NEC Online TV
    • Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Ratiba ya Kampeni za Wagombea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, 2020
    • Voters Interaction System
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Jarida la Tume la Uchaguzi Mkuu 2020
  • Zabuni/Mnada
    • Zabuni za Ndani
    • Zabuni za Kimataifa
  • Mawasiliano
  • Jarida la Uchaguzi

Tume yatangaza Siku ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020

Imewekwa: July 21, 2020

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza siku ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani wa Tanzania Bara kuwa ni siku ya Jumatano ya tarehe 28 Oktoba mwaka huu 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji Rufaa (Mst.) Semistocles Kaijage, amesema Uteuzi wa Wagombea Kiti cha Rais na Makamu wa Rais, Ubunge, na Udiwani utafanyika tarehe 25 Agosti, 2020 na kampeni za Uchaguzi zitaanza tarehe 26 Agosti, 2020 hadi 27 Oktoba mwaka huu wa 2020.


Alisema Tume imetoa taarifa hiyo chini ya Ibara ya 41(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ikisomwa pamoja na vifungu vya 35B (1), (37) (1) (a) na 46 (1) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na kifungu cha 48 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.


“Tume inapenda kuutarifu Umma kuwa Ratiba ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani wa Tanzania Bara itakuwa kama ifuatavyo.Uteuzi wa Wagombea Kiti cha Rais na Makamu wa Rais, Ubunge, na Udiwani utafanyika tarehe 25 Agosti, 2020, kampeni za Uchaguzi zitaanza tarehe 26 Agosti, 2020 hadi 27 Oktoba mwaka huu wa 2020 na Siku ya Uchaguzi itakuwa tarehe 28 Oktoba, 2020”alisema Jaji Rufaa (Mst) Kaijage.


Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani wa Tanzania Bara kwa mwaka huu wa 2020, unakuja baada ya uchaguzi kama huo uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka 2015.

Habari Mpya

  • Tume yatangaza matokeo ya Uchaguzi Jimbo la Mbarali na Kata Sita za Tanzania Bara
    September 21, 2023
  • ?Mwenyekiti wa Tume Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele atembelea na kukagua Uchaguzi Mdogo Jimbo la Mbarali
    September 19, 2023
  • Wapiga kura 216,282 kupiga kura uchaguzi mdogo wa Mbarali na kata sita
    September 19, 2023

Nifanyaje?

  • Kujiandikisha Kupiga Kura
  • Kupiga Kura

Machapisho

  • Jarida la Uchaguzi, Agosti, 2023
  • Jarida la Uchaguzi Toleo la Julai, 2023
  • Jarida la Uchaguzi Toleo la Machi, 2023
  • Jarida la Uchaguzi Toleo la Februari, 2023
  • Jarida la Uchaguzi Toleo la Januari, 2023
Tanzania Census 2022

Mawasiliano yetu

  • Address : P.O.Box 358, Dodoma, The National Electoral Commission, 5 Uchaguzi Road, 41107 Njedengwa Uchaguzi House
  • Namba ya Simu : +255 26 2962345-8
  • Nukushi : +255 26 2962348
  • Barua Pepe : uchaguzi@nec.go.tz
  • Tovuti : www.nec.go.tz

Linki za Haraka

  • Maktaba ya Tume.
  • Majukumu ya Msingi

Tovuti Mashuhuri

  • Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Bunge la Tanzania
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu
  • Msajili wa Vyama vya Siasa

Kuwa karibu nasi

Jiunge na orodha ya baruapepe zetu ili uhabarishwe na kupata notisi kuhusu taarifa zetu mpya

Tufuatilie

@2023 Tume ya Taifa ya Uchaguzi . Haki zote zimehifadhiwa

  • Ramani ya Tovuti
  • Wasiliana Nasi