Mwenyekiti NEC afungua mafunzo kuwajengea uwezo wajumbe wapya na maafisa wa Tume za SADC
Imewekwa: November 22, 2022
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inashiriki mafunzo ya siku nne ya kuwajengea uwezo wajumbe wapya na maafisa waandamizi wa Tume za Uchaguzi wa Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Mafunzo hayo yaliyofunguliwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele, yanafanyika kupitia
Jukwaa la Tume za Uchaguzi za Nchi Wanachama wa SADC (ECF-SADC).
Washiriki wa mafunzo hayo wanajumuisha wajumbe wapya wa Tume
za Uchaguzi na maafisa kutoka nchi tisa wanachama wa jukwa ambazo ni mwenyeji
Tanzania, Zambia, Eswatini, Ushelisheli, Botswana na Namibia.
Nchi nyingine zinazoshiriki ni Zimbabwe, Lesotho, na Malawi ambapo mafunzo hayo yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 25 Novemba, 2022.