Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango apata mrithi Ubunge Jimbo la Buhigwe
Imewekwa: May 17, 2021
Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buhigwe Felix Kavejuru amepata ushindi katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo baada ya kupata kura nyingi zaidi ya wagombea wengine.
Msimamizi wa
Uchaguzi wa Jimbo la Buhigwe Bi. Marycelina Mbehoma amemtangaza Bw. Kavejuru kuwa
mshindi baada ya kupata kura 25,274 ksti ya kura 30320 halali zilizopigwa.
.
Akitangaza matokeo
ya uchaguzi huo Bi. Marycelina Mbehoma alisema Bw. Kavejuru aliwashinda wagombea
wenzake kutoka vyama 12 vya siasa vilivyoshiriki katika uchaguzi huo.
Baada ya
kutangaza matokeo ya uchaguzi huo Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Muhambwe, Bi.
Marycelina Mbehoma alimkabidhi cheti cha ushindi Bw. Kavejuru kama
inavyoelekezwa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.
Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Buhigwe ulifanyika Mei 16 mwaka 2021 pamoja na Uchaguzi Mdogo wa Ubunge Jimbo la Muhambwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo mkoani Kifoma na Uchaguzi wa Madiwani katika Kata Tano za Tanzania Bara.
Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Buhigwe ulifanyika baada ya mbunge wa jimbo hilo (Dkt. Philip Mpango kupoteza sifa za kuwa mbunge baada ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.