Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
• Mfumo wa Uandikishaji Wapiga Kura wa hapo awali (OMR) ulionekana kupitwa na wakati na hivyo kuwa vigumu katika uhifadhi wa taarifa zake.
• Taarifa za kimaumbile (Bio metric Features) zinazochukuliwa zinatumika katika kulinganisha taarifa za watu mbalimbali na hivyo kuzuia watu kuwepo mara mbili katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.• Kadi Imara ya Mpiga kura
Uchaguzi wa Rais
Uchaguzi wa Wabunge
Uchaguzi wa Madiwani Tanzania Bara
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ina majukumu yafuatayo:
(a) Kusimamia na Kuendesha Uandikishaji wa Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
(b) Kusimamia na Kuendesha Uchaguzi wa Rais na Wabunge katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
(c) Kupitia na Kugawa Mipaka ya Jamhuri ya Muungano katika Majimbo mbali mbali
ya Uchaguzi wa Wabunge.
(d) Kusimamia na Kuendesha Uandikishaji wa Wapiga Kura na kuendesha Uchaguzi wa
Madiwani Tanzania Bara.
(e) Kutangaza matokeo ya Viti Maalum vya wanawake vya Ubunge na Udiwani. ;
(f) Kutoa Elimu ya Mpiga Kura na kusimamia Watu na Asasi zitakazohusika katika
Kutoa Elimu hiyo.
(g) Kutekeleza Majukumu mengine yatokanayo na Sheria itakayotungwa na Bunge.