Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara
Atatangazwa kama Mgombea asiye na Mpinzani na hivyo kuwa amechaguliwa
Uteuzi ni sehemu ya Mchakato wa Uchaguzi,ambapo Mgombea anachaguliwa na chama chake kugombea nafasi katika Uchaguzi
Ndio, Mawakala wa Vyama vya Siasa vyenye Usajili wanaruhusiwa kuwa na mwangalizi mmoja kwa kila kituo cha Uandikishaji Wapiga kura .
Ni kosa la Jinai mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja, na ikitokea, mtu ataadhibiwa kulingana na Sheria za Uchaguzi.
• Ikiwa ana Uraia wa Nchi nyingine yaani sio Raia wa Tanzania,
• Amehukumiwa kifungo cha zaidi ya Miezi Sita,• Amehukumiwa kifo na Mahakama za Tanzania,
• Amethibitika kuwa hana Akili timamu.
Hakuna Nyaraka zozote zinazohitajika wakati wa Uandikishaji, Ijapokuwa kwa wale Wapiga Kura wenye Vitambulisho vya Upigaji Kura wanatakiwa kumkabidhi Mwandikishaji Msaidizi kadi yake ili kurahisisha zoezi la Uandikishaji.
Katika kituo cha Uandikishaji Wapiga Kura kilichopo jirani na eneo unaloishi.
Kipindi cha Uandikishaji Wapiga Kura katika eneo lako kitatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Vyombo vya Habari , Radio, TV na Magazeti.
Raia yeyote wa Tanzania aliyetimiza Umri wa miaka 18 na kuendelea na yule atakayetimiza Umri wa Miaka 18 Oktoba 2015 anafaa kuandikishwa kuwa Mpiga Kura.
• Ili kuweza kutimiza haki yako katika Kupiga Kura siku ya Kura ya Maoni na Uchaguzi.
• Kuweza kushiriki katika uongozi Nchi yako.