Uteuzi wa Wagombea Urais
Imewekwa: 2015-08-21 18:08:46
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeteua wagombea
wa Urais kutoka vyama nane ambao
wametimiza vigezo vilivyowekwa na Tume walioomba nafasi ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jumla ya Vyama Kumi na vitatu (13)
vilichukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea Urais katika Ofisi za Tume ya Makao Makuu ya Tume tangu zoezi hilo lilipoanza rasmi Agosti 1,2015.
Wagombea wa Urais waliochukua fomu
walitakiwa kutimiza matakwa ya kisheria ikiwa ni pamoja na kupata wadhamini
wasiopungua mia mbili (200) waliojiandikisha Kupiga Kura kila mkoa kwa mikoa
kumi kati ya hiyo,miwili iwe ya Tanzania Zanzibar, pamoja na kuweka dhamana ya shilingi milioni
moja na kula kiapo mbele ya Jaji wa Mahakama.
Hadi kufikia Saa kumi kamili jioni ya leo
tarehe 21 mwezi Agosti, 2015 jumla ya Vyama tisa (9) Vilikuwa vimewasilisha
fomu zikiwa zimekidhi vigezo vilivyotajwa na kwa hatua hiyo Wagombea wao
kuteuliwa rasmi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa wagombea halali wa Nafasi ya
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vyama vilivyokuwa vimewasilisha fomu katika
Tume ya Taifa ya Uchaguzi hadi kufikia saa kumi kamili jioni ni kama ifuatavyo:
1. Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
2. Chama
cha Mapinduzi (CCM)
3. Chama
cha Tanzania Labour Party (TLP)
4. Chama
cha Alliance Democratic (ADC)
5. Chama
cha United People’s Democratic Party (UPDP)
6. Chama
cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA)
7. Chama
cha Alliance for Change and Transparent (ACT-WAZALENDO)
8. National
Reconstruction Alliance (NRA)
9. Chama
cha African Democratic Alliance (ADA-TADEA)
Kwa hatua hii na kwa mujibu wa Sheria, Tume
ya Taifa ya Uchaguzi inawatangaza Wagombe wafuatao pamoja na Vyama vyao kuwa
ndio Wagombea Halali wa nafasi ya Urais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania:
1. Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Mhe. Edward Ngoyai Lowassa
2. Chama
cha Mapinduzi (CCM)
Mhe. John Pombe Magufuli
Samia Suluhu Hassan
3. Chama
cha Tanzania Labour Party (TLP)
Machmillan Elifatio Lyimo
4. Chama
cha Alliance Democratic (ADC)
Chief Lutalosa Yembe
Mhe. Said Miraj Abdallah
5. Chama
cha United People Democratic Party (UPDP
Mhe. Fahmi Nassoro Dovutwa
Hamadi Mohammed Ibrahimu
6. Chama
cha UMMA (CHAUMMA)
Hashim Rungwe Spunda
Issa Abas Hussein
7. Chama
cha Alliance for Change and Transparent (ACT-WAZALENDO)
Anna Elisha Mghwira
Hamad Mussa Yussuf
8. National
Reconstruction Alliance (NRA)
Janken Malik Kasambala
Simai Abdulrahman Abdulla
Kwa kuzingatia Idadi ya Vyama vilivyochukua
fomu ambavyo ni kumi na vitatu, dhidi ya vyama tisa (9) vilivyorejesha fomu
ndani ya muda yaani kati ya saa 1.30 asubuhi na saa 10.00 jioni, vyama viwili vimeshindwa
kurejesha fomu kwa wakati wakati ambapo vyama vingine viwili vimeshindwa
kukamilisha masharti.
Chama
cha Kijamii (CCK) na Chama cha African Democratic Alliance Party (ADA-TADEA)
vimerejesha fomu lakini havikuweza kukidhi matakwa kwa mujibu wa sheria
wakati Chama cha Haki na Ustawi
(CHAUSTA) na Chama cha Democratic Party (DP) havikurejesha kabisa fomu.
Kwa Chama cha CCK kimeshindwa kukamilisha
fomu namba 8 inayoonyesha idadi ya wadhamini wanaotakiwa kwa mujibu wa sheria.
Aidha Chama cha ADA TADEA hakikukamisha sharti la Mgombea Mwenza kula kiapo.
Chama cha DP kimeshindwa kukidhi vigezo ikiwemo kuwa na Mgombea Mwenza pamoja na kulipa dhamana inayotakiwa.

